Big Sean: namdai Kanye West zaidi ya bilioni 13.8

Big Sean: namdai Kanye West zaidi ya bilioni 13.8

Baada ya hivi karibuni Msanii kutoka nchini Marekani Kanye West kusema anajuta kumsaini katika label yake msanii Big Sean, unaambiwa Sean amedai kuwa anamdai Rapa huyo zaidi ya Bilioni 13.8.

Big Sean kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa madai hayo baada ya shabiki wake aliyesema kwamba (Big Sean) anamdai Kanye takribani Bilioni 6.9 na yeye kujibu anamdai zaidi ya Bilioni 13.8.

Juzi Kanye alitoka adharani na kusema kuwa katika vitu anavyojuta ni kumsajili Big Sean katika label yake ya muziki.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags