Binti wa Eminem afunga ndoa

Binti wa Eminem afunga ndoa

Binti wa ‘rapa’ kutoka nchini Marekani Eminem, Hailie Jade Scott, ameripotiwa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Evan McClintock ndoa hiyo iliyofungwa wikiend hii ambayo ilihudhuriwa na ndugu pamoja na marafiki wa karibu tu.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Hailie Jade Scott, alilithibitisha hilo kwa kushare baadhi ya picha zake za harusi moja wapo ikiwa ni picha akicheza muziki na baba yake katika sherehe hiyo.

Wanandoa hao wapya walikutana kwa mara ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan mwaka 2016 na kuchumbiana Februari 2023.

Eminem alimpata binti huyo kutoka kwa mke wake wa zamani Kim Scott ambapo wawili hao walianza uhusiano mwaka 1989 na walifunga ndoa 1999 na kuachana miaka miwili baadaye , kisha kuoana tena mwaka 2006 na kuachana tena miezi michache baada ya ndoa yao kupita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags