Akon Alikuwa Akimtumia Mdogo Wake Kufanya Show

Akon Alikuwa Akimtumia Mdogo Wake Kufanya Show

Mwanamuziki na mwigizaji kutoka Senegal ambaye anaishi Marekani, Akon Thiam amethibitisha kuwa mdogo wake aitwaye Abou "Bu" Thiam alikuwa akimuwakilisha kwenye baadhi ya matamasha yake wakati alipokuwa amebanwa na kazi nyingi.

Wakati alipokuwa kwenye mahojiano na The Morning Hustle, aliweka wazi kuwa kipindi alipokuwa anahit kupitia muziki wake alikuwa na ratiba ngumu hivyo alimtumia mdogo wake kukamilisha baadhi ya matamasha ambayo asingeweza kufika.

“Bu alikuwa 'double' wangu. Hii ilikuwa kabla ya mitandao ya kijamii. Kama ungeona Abou mahali pamoja na mimi mahali pengine, usingeweza kutofautisha,”amesema Akon

Akon alieleza kuwa Bu alianza kama "hype man" wake, lakini kutokana na maombi mengi ya maonesho, aliamua kumtumia kama mwakilishi wake ili maokoto yasipotee. Bu hakuwa na uwezo wa kuimba, hivyo DJ alikuwa akimuwekea ngoma za kaka yake huku Bu akifanya "lip sync" jukwaani.

Pia alifichua kuwa ndugu yake mwingine, Omar, aliwahi kujifanya kuwa yeye bila ruhusa, akifanya maonesho katika miji na nchi mbalimbali, jambo ambalo lilimshangaza Akon alipojua kuwa tayari "alikuwa amewekewa ratiba" katika maeneo hayo.

Akon alisisitiza kuwa katika enzi hizo, kabla ya mitandao ya kijamii, mashabiki hawakuweza kutofautisha kati yake, Bu na Omar, hasa kwa sababu walifanana sana, na tofauti pekee ilikuwa kwamba Bu alivaa kofia wakati Akon hakuwa na desturi hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags