AZIZ KI NA MOBETTO SASA NI MKE NA MUME

AZIZ KI NA MOBETTO SASA NI MKE NA MUME

Baada ya kuzuka kwa tetesi nyingi kuhusiana na harusi ya nyota wa Yanga na Mwanamitindo Hamisa Mobetto, hatimaye ndoa ya wawili hao tayari imeshapita.


Ndoa hiyo imefungwa na Shekh mkuu wa Dar es Salaam, Shekh Walid Alhad Omar na mashekh wengine katika Msikiti uliopo Mbweni leo Februari 16,2025 jijini Dar es Salaam.


Akizungumza baada ya ndoa hiyo kupita Shekh Walid amewatakia kheri wanandoa hao huku akisisitiza watu kuepuka Zinaa.


Baada ya kufunga ndoa lakini pia kutakuwa na sherehe nyingine ambayo itafanyika Februari 19 kwenye ukumbi wa Superdome Masaki Jijini Dar es Salaam.


Mapema Jana Hamisa Mobetto, Februari 15, 2025, amelipiwa mahari ya ng'ombe 30 na kiasi cha Sh 30 milioni na Stephanie Azizi Ki ambaye ni kiungo mshambuliaji ya Yanga.



Hii itakuwa ndoa ya kwanza kwa wanandoa hao huku Hamisa akiwa na watoto wawili kutoka kwa baba tofauti ambapo mtoto wa kike amezaa na Mkurugenzi wa EFM Francis Majizo na wa kiume supastaa wa Tanzania Diamond Platnumz, lakini kwa upande wa Aziz Ki anamtoto mmoja wa kike ambaye amekuwa akimpoati kupitia mitandao ya kijamii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags