Costa Titch Muda Mchache Mambo Makubwa

Costa Titch Muda Mchache Mambo Makubwa

Nani kama Costa Titch? muda aliohudumu kwenye muziki ni mchache lakini alifanikiwa kuonesha kila juhudi na mafanikio kwenye kazi yake. Costantinos Tsobanoglou maarufu kama Costa Titch mzaliwa wa Afrika Kusini alijizoelea umaarufu kupitia muziki wa amapiano na uwezo wake wa kulitawala jukwaa kwa kuimba na kucheza.

Msanii huyo ambaye alifariki dunia Machi 11, 2023, baada ya kuanguka jukwaani kwenye tamasha la Ultra South Africa music festival lilofanyika Johannesburg, South Afrika hakuwa na muda mwingi kwenye tasnia ya burudani tangu kuanza kwake mwaka 2020 baada ya kuachia album yake ya kwanza ya mtindo wa Hiphop inayofahamika kama 'Made In Afrika' ikitawaliwa na collabo za wasanii wakubwa kutokea Afrika Kusini kama AKA, Riky Rick, na Boity.

Licha ya album hiyo kukosolewa lakini ilifanikiwa kupata mauzo mazuri sokoni na kufanikiwa kumuweka msanii huyo kwenye nafasi nzuri kama moja ya mastaa chipukizi kwenye kiwanda cha muziki Afrika.

Mafanikio hayo yalipelekea mpaka kutambulika kwenye Tuzo za muziki wa Hiphop Afrika Kusini akifanikiwa kutokea kwenye vipengele vitatu na kushinda wimbo bora wa kushirikiana kupitia wimbo wa 'Nkalakatha Remix' aliowashirikisha AKA and Riky Rick.

Lakini pia, kupitia wimbo wa 'Ayeye' wa kwake Major League DJz, Abidoza ambao Cost alishirikishwa ulipokelewa vizuri kutokana na ujumbe wake ambao uliwateka mashabiki wengi. Costa Titch aliendelea kutoa ngoma kubwa na kali ikiwemo Big Flexa ambayo imeweka rekodi ya kuwa wimbo wa amapiano ambao umetazamwa mara nyingi zaidi kwenye mtandao wa YouTube ukitazamwa zaidi ya mara milion 128.

Kwenye Spotify wimbo huo umesikilizwa zaidi ya mara Milioni 17. Wakati wa enzi za uhai wake Costa alifanikiwa kufanya kazi na msanii kutokea Marekani mwenye asili ya Senegal, Akon ambaye walifanya remix ya wimbo wake wa Big Flexa.

Hata hivyo, msanii huyo alifanikiwa kufanya kazi na wasanii tokea Tanzania akiwemo Diamond Platnumz ambaye walishirikiana kupitia wimbo wa Superstar ambao video yake iliachiwa Oktoba 7, 2022, ukifanikiwa kutazamwa mara milioni 22 Youtube. Novemba 23, 2022 alishirikishwa na Mbosso kwenye wimbo wa Shetani ambao umetazamwa mara milion 17 kwenye mtandao wa Youtube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags