Wakati wewe ukilalamika watu kutokupigia simu kwa siku mbili au moja na kujiita mpweke kwa upande wa Joyce Carol Vincent, raia wa Uingereza mwenye miaka 38, anatajwa kuwa ndio alikuwa mwanamke mpweke zaidi duniani ambapo alipatikana amefariki dunia nyumbani kwake miaka mitatu baada ya kifo chake.
Joyce, ambaye alikuwa akifanyakazi katika kampuni kubwa ya kifedha, alikuwa akifahamika kwa uchangamfu, upendo kwa marafiki na mwenye ndoto alikutwa amefariki akiwa ameketi kwenye sofa lake huku televisheni ikiwa bado inawaka na zawadi za Krismasi zikiwa hazijafunguliwa.
Inaelezwa kuwa Joyce alifariki Desemba 2003 kutokana na matatizo ya kiafya ambayo ni Asma na vidonda vya tumbo ambapo mwili wake uligunduliwa Januari 2006 ikiwa ni miaka mitatu baada ya kifo chake hali iliyoonesha jinsi alivyokuwa mpweke na mtu ambaye amejitenga na jamii.
Wiki zikapita miezi harufu iliyodumu kwenye kodro kwa muda mrefu ilipuuzwa ikihusishwa na mapipa ya taka. Hatimaye fedha ziliisha kwenye akaunti yake, mwenye nyumba alituma barua za kudai pesa ya kodi lakini hakupatiwa majibu ndipo mahakama ikatoa amri ya kumtoa ndani ambapo walivunja mlango na kukuta mabaki yake.
Wakati wa uhai wake, Joyce alikuwa mtu mwenye hadhi ambaye alikutana na watu mashuhuri akiwemo Nelson Mandela na Stevie Wonder. Kwa mijibu wa vyombo vya habari mbalimbali vinaeleza kuwa wakati wa mwisho wa maisha yake mwanadada huyo alijitenga na marafiki, familia jambo ambalo lilipelekea kutokea kwa kifo chake bila watu kugundua kwa muda mrefu.
Aidha kufuatia na tukio hilo mwongozaji wa filamu nchini humo Carol Morley aliachia filamu maalumu kuhusu miasha ya Joyce iitwayo ‘Dreams of a Life’ (2011) ambapo filamu hiyo ilizua mijadala katika mitandao ya kijamii huku jamii ikimtaja kuwa alikuwa ndie mtu mpweke zaidi.
Hata hivyo baadhi ya wadau mbalimbali wameilaumu familia pamoja na marafiki wa Joyce kwa kumtenga kwa kipindi chote, kutokana na tukio hilo wataalamu wa afya ya akili wameendelea kusisitiza umuhimu wa wa kuwa na uhusiano wa karibu, kujali wengine.

Leave a Reply