Kabla Ya Kuigiza Juakali Judith Alikuwa Model

Kabla Ya Kuigiza Juakali Judith Alikuwa Model

Judith Actress, ndilo jina la Mwanadada anayekuja kwa kasi na kuwabamba mashabiki wa filamu nchini. Sio tu kwa uwezo wake wa kuifanya sanaa pia kwa muonekano wake.

Quruthum Athuman ndio jina alilopewa na wazazi, nyota yake imeng’aa zaidi kutokana na tamthilia ya Juakali ambayo anaicheza.

Siku za hivi karibuni Judith ameendelea kujizolea umaarufu kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakisifia mwonekano wake.

Akizungumza na Mwananchi Scoop mwigizaji huyo amesema kabla ya kuonekana kwenye Jua Kali tayari alikuwa amepita kwenye vikundi mbalimbali vya kuigiza ambako ndiko alikutana na mwigizaji mwenzie Isarito Mwakalindile.

"Tamthilia yangu ya kwanza ni Juakali na nilianza kuigiza mwaka 2021, uwezo na mwonekano wangu ndio ulifanya Lamata na Isarito nifanye nao kazi," Amesema Judith.

Kutokana na mwonekano wake ambao amekuwa akisifiwa nao Judith amesema miaka mitatu iliyopita alikuwa akijihusisha na masuala ya fashion na urembo na alibahatika kushiriki majukwaa mbalimbali yaliyomfanya anyakuwe tuzo kadhaa.

"Nilikuwa nafanya masuala ya fashion na umodo miaka mitatu nyuma lakini sasahivi nimeacha nimefanya kwenye majukwaa kama Red In Red Swahili Fashion Stara Fahion na nimepata tuzo mbili kwenye Stara fashion na Creativity Fashion," amesema Judith.

Hata hivyo ameongezea kuwa urembo wake ni changamoto kwa sasa kwani amekuwa akipambanishwa na wanawake wengine kwenye tasnia ya burudani.

"Changamoto ninayoipata kwasasa ni watu kujilinganisha na mimi wanashindwa kuelewa kuwa mimi siwezi kuwa kama wao na wao hawawezi kuwa kama mimi wanashindwa tu kuelewa.

“Katika picha zote mbili zinazosambaa mitandaoni sikupaka kipodozi chochote kwenye uso wangu na sijajua kwanini wamezifananisha zile picha mimi sikupiga picha ili ni zilinganishe ," amesema Judith.

Kama wasemavyo waswahili kulinda brand ni muhimu, ndivyo mwigizaji anasema mara yake ya mwisho kupanda daladala ni miaka nyuma iliyopita.

Judith amejitabiria makubwa nadani ya miaka mitatu ijayo akijiwazia kuwa na biashara yake. Lakini Licha ya mwanadada huyo kupenda masuala ya fashion amesema hatazamii kufungua biashara ya nguo kabisa.

"Napenda mavazi lakini sitamanii kufanyia biashara kabisa," amesema Judith.

Wakati baadhi ya watu wakiwa wanasherehekea Valentine day Judith amesema yeye hafagilii kabisa mwezi huu

" Sina Valentine na siku hiyo huwa nachukulia siku kama siku nyingine tu. Hata mpenzi wangu niliyekuwa naye nyuma hatukutoboa hata Valentine na kwenye maisha yangu nimewahi kupitia mahusiano mara moja tuu mpaka sasa nipo single," amesema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags