Kauli ya mwisho ya Carina kwa mdogo wake

Kauli ya mwisho ya Carina kwa mdogo wake

Mdogo wa marehemu Hawa Hussein (Carina), Saphinewi Salvan amesema dada yake alimuahidi akirudi nchini atawaasili (adopt) watoto wake kisheria.

“Tarehe 14 tuliongea sana kila wakati alikuwa ananipigia simu. Alikuwa anasema mimi nataka leo tuongee, tukawa tunaongea video call akawa amesimama anapika. Ananiambia leo nataka kula chakula ambacho nimekipika mwenyewe.

"Nikamsifia amependeza, amekuwa mzuri sana. Akaniambia rangi yangu ni nzuri sana labda nakufa utajuaje, nikamwambia acha maneno yako bwana. Akaniambia nikirudi nataka niwaasili watoto wako kisheria sitaki uniingilie kwenye malezi yangu," amesema Saphinewi

Mdogo huyo wa marehemu aliendela kuonesha majonzi yake kwa kudai huenda angekuwa karibu na dada yake angemuwahisha hospitali.

"Najuta kwanini nilirudi natamani ningekuwepo ningemwambia dada yangu twende hospitali, labda angenikubalia kwa sababu waliokuwepo naye, wanasema tulikuwa tunamwambia tumpeleke hospitali lakini aliwaambia wataenda saa 1,”

Carina ambaye alifariki dunia Aprili 15,2025 nchini India alipoenda kupatiwa matibabu, ameacha mtoto mmoja wa kike aitwaye Aisha mwenye umri wa miaka 16.


Utakumbuka carina alionekana kama Video Queen kwenye wimbo wa ‘Oyoyo’ wa kwake Bob Junior lakini pia alicheza kwenye tamthilia ya kwanza ya mwigizaji Jacob Stephen ‘JB’ ya mwaka 2017 hadi 2018 iliyoitwa ‘Kiu ya Kisasi’.

🎤 @officialtinana
🎥 @nyembe_b46

Video kamili ipo YOUTUBE ya MWANANCHI DIGITAL.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags