Endapo jana Februari 14 ulikosa raha kwa sababu wengi walisherehekea siku ya wapendanao kwa kupokea zawadi, ujumbe wa mahaba au kwenda matembezi na wenza wao, wakati wewe hauna mwenza, basi leo ndiyo siku yako.
Kama ambavyo jana dunia iliadhimisha siku ya wapendanao leo inaadhimishwa siku watu wasiokuwa na wenza, kwa maana nyingine inawezekana, wapo wanaowapenda lakini si wa uhusiano wa kimapenzi.
Siku hii inayofahamika kama Single Awareness Day (Siku ya kutambua upweke katika mahusiano) huadhimishwa Februari 15, siku moja baada ya kuadhimishwa Valentine.
Maadhimisho haya si kwamba yanahamasisha watu wawe wapweke, la hasha.
Yanalenga kuwafanya wasio na wapenzi waelewe maana yake na wasijione kwamba kuwa katika hali hiyo ni mwisho wa maisha kwao.
![Leo Ni Siku Ya Wasiokuwa Na Wapenzi Duniani](https://mwananchiscoop.co.tz/public/uploads/2025/02/15/fr69373e672a4c6969b282f87fc1608f8d4ff4c301.jpeg)
Leave a Reply