Siku ya Emoji Duniani ilianzishwa rasmi Julai 17, 2014 na Jeremy Burge, mwanzilishi wa tovuti ya Emojipedia.
Katika kipindi cha miaka michache, siku hii imekuwa maarufu duniani kote, huku makampuni na majukwaa yakitumia fursa hiyo kuzindua emoji mpya au kufanya kampeni maalum zinazohusisha alama hizo.

Mbali na kutoa burudani, wataalamu wa mawasiliano wanasema emoji zimeleta mapinduzi katika lugha ya mtandaoni, zikisaidia kupunguza tafsiri potofu na kuongeza maelewano ya kihisia katika mazungumzo.
Aidha mpaka kufikia sasa Emoji maarufu zaidi duniani ni ‘😂 Face with Tears of Joy’ 😂 Uso Wenye Machozi ya Furaha ambayo inawakilisha furaha kupitiliza na kicheko kisichoweza kudhibitiwa, imekuwa ikiongoza mara kwa mara kwenye orodha ya emoji maarufu zaidi duniani.
Hivyo basi ili kuadhimisha siku hii basi unaweza kuwatumia marafiki, ndugu na jamaa emoji ambayo unaipenda zaidi lakini pia unaweza kuiadhimisha kwa kuvaa mavazi yenye alama za emoji.
Leave a Reply