Mfahamu Mwanaume Aliyetafuna Ndege Aina Ya Cessna 150

Mfahamu Mwanaume Aliyetafuna Ndege Aina Ya Cessna 150

Michel Lotito maarufu Monsieur Mangetout ‘Bwana mla kila kitu’ kutoka Ufaransa aliingia katika kitabu cha Rekodi ya dunia Guinness, baada ya kuweka rekodi ya mtu anayekula vitu visivyo vya kawaida.

Lotito alijulikana zaidi kwa kula vitu vya chuma ikiwa ni pamoja na baiskeli, televisheni, Pikipiki huku akiwashangaza wengi kwa uamuzi wake wa kula ndege nzima aina ya Cessna 150.

Kulingana na madaktari, mtu huyo alikuwa na mfumo wa mmeng’enyo wa chakula wenye uwezo wa kipekee, ambapo ukuta wa tumbo lake ulikuwa mnene zaidi ya kawaida na asidi ya tumbo lake ilikuwa na nguvu kubwa ya kuyeyusha vyuma.

Mwanaume huyo anadaiwa kula vitu aina ya chuma kilo moja kwa siku nzima na ili kuwa sawa alikuwa akitumia mafuta ya kulainisha vyuma hivyo na kunywa maji mengi ili kupata choo bila matatizo.

Michel Lotito aliingia kwenye Kitabu cha Rekodi za Guinness kwa kula ndege nzima aina ya Cessna 150, jambo ambalo lilimchukua takriban miaka miwili (1978–1980) kukamilisha.

Aidha hakuwahi kupata matatizo makubwa ya afya kutokana na tabia yake ya kula vitu hivyo ambayo alianza kula akiwa na umri wa miaka 9 akila vitu kama udongo, vipande vya kioo, na karatasi.

Michel Lotito ambaye alizaliwa 15 Juni 1950 alifariki dunia 25 Juni 2007 akiwa na umri wa miaka 57. Kifo chake kilitokana na matatizo ya afya yanayohusiana na umri na si kwa sababu ya tabia yake ya kula vitu visivyo vya kawaida.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags