Obama aliandika ujumbe kupitia mitandao yake ya kijamii uliokuwa ukieleza “Miaka thelathini na miwili pamoja na bado unanifanya nikose pumzi. Heri ya Siku ya Wapendanao,”
Chapisho hilo lilipata komenti mbalimbali ambapo watu walikuwa wakiwapongeza wawili hao kwenye kila hatua “Ninyi wawili ni mfano wa kuigwa. Asanteni. Heri ya Siku ya Wapendanao,”,
![](../../public/uploads/2025/02/15/fr73414b3b14a66f31c372654fee6b2db40fcff719.jpeg)
“Heri ya wapendanao kwa wanandoa wapendwa zaidi. Tunawapenda na tunawakosa sana!”, huku wengine wakiongeza utani wakiandika “Nataka mapenzi yenye nguvu kama yao lol!,”. mbali na hao wengi wao walionekana kupendezwa na ndoa ya wawili hao ambayo imedumu kwa muda mrefu.
Aidha chapisho hilo limekuja kutuliza uvumi wa madai ya kuwa wawili hao wanamapngo wa kupeana talaka. Barack na Michelle Obama walifunga ndoa 3 Oktoba, 1992 huku wakijaaliwa kupata watoto wawili ambao ni Malia Obama (aliyazaliwa mwaka 1998) na Sasha Obama (aliyazaliwa mwaka 2001).
Leave a Reply