Burna Boy Atoa Maelezo Sababu Ya Kushuka Stejini

Burna Boy Atoa Maelezo Sababu Ya Kushuka Stejini

Mkali wa Afrobeat, Burna Boy ametoa maelezo sababu ya kushuka jukwaani baada ya shabiki kumvamia kwa kudai kuwa muda wake ulikuwa tayari umekwisha.

Utakumbuka kuwa msanii huyo alisusia Show hiyo iliyofanyika Desemba 31, 2024 baada ya shabiki mmoja kumvamia jambo ambalo liliwaacha njia panda mashabiki, aidha kupitia Instagram ya Burna ameshare ujumbe akidai kuwa muda wake wa kufanya show ulishaisha.

“Ilikuwa ni show ya bure, nilitakiwa kuifanya kwa dakika 10 lakini nikaifanya kwa saa zima, muda wangu ulikuwa umshakwisha,” ameandika Burna Boy.

Mbali na hilo lakini pia Burna aliwataka baadhi ya mashabiki wanaopendelea kupanda jukwaani wakati anatumbuiza kuacha tabia hiyo kwani hapendezwi nayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags