Cardi B Alichepuka kipindi cha ujauzito

Cardi B Alichepuka kipindi cha ujauzito

Rapa kutoka Marekani Offset amedai aliyekuwa mkewe na mzazi mwenzie Cardi B aliwahi kuchepuka kipindi akiwa na ujauzito wa mtoto aliyejifungua hivi karibuni.

Offset ameyazungumza haya wakati Cardi alipokuwa live kupitia Instagram yake akimtaka rapa huyo aongee ukweli kama alichepuka wakati wa ujauzito.

“Una mahusiano na mtu mwingine huku ukiwa mjamzito, sema ukweli” ambapo Cardi alijibu kwa haraka kwenye mtandao wa X akisema ‘Ndio Nilifanya’.

Hayo yanakuja baada ya Cardi kudai kuwa Offset amekuwa akichukua vitu vyake na kumpelekea mpenzi wake mpya.

“Kama unataka kucheza michezo hii na mimi, basi tutaicheza pia kwa kuwa unataka kunitishia kwa kusema unakusudia kuchukua vitu vyangu kwa sababu naendelea na maisha yangu, basi endelea kwa nini ni vigumu sana kwako kuendelea?” alisema Cardi

Mahusiano kati ya Cardi B na Offset yamekuwa na migogoro mingi, walipeana talaka kwa mara ya kwanza 2020 lakini baadaye walikuja kusuluhisha matatizo yao, hata hivyo uhusiano wao ulianza kutetereka tena mwishoni mwa mwaka jana.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags