Chanzo Cha Neno Wanaume Wote Ni Mbwa

Chanzo Cha Neno Wanaume Wote Ni Mbwa

Kujenga nyumba ni rahisi sana kama ukiwa hatua za mwanzoni. Urahisi wenyewe huanzia kwenye lugha na maongezi yake. Yaani ni kisiwahili mwanzo mwisho.

Kiwanja, mchanga, msingi, kokoto, tofari, nondo, misumari, maji, zege, mbao, nyundo, chepeo, mawe nk. Vyote hivyo hutamkwa kwa lugha yetu ya Kiwalani.

Sasa ngoja ifikie hatua ya kubadili lugha kutoka kiswahili hadi ngeri.
Plaster, gypsum, grill, blandering, skiming, painting, wiring, tiles, toilets sink, aluminium sijui nini sijui…

Hapo ndo unasikia mtu kaishia kwenye rinta na kuacha yawe makazi rasmi ya popo. Na kwenye mapenzi ni kinyume chake. Lugha ya mwisho huwa mwanzo na ya mwanzo huwa mwishoni.

Mwanzoni kwenye mapenzi mara nyingi huanza na viingereza vingi. Unaweza kudhani ni wakazi wa London Town. Sweetie, Darling, Baby, Honey, Daddy, Boo, My love, na kwa simu utaseviwa My Heart au wife kabisa…

Sasa subiri pindi wakizoeana sana, na penzi kuanza kupukutika. Lugha hubadilika na kurudi kwenye asili yake. Huanza kuitwa kwa jina halisi la Ashura Kipopole na kwenye simu ataseviwa ‘kimeo’.

Simu hazipokelewi na zikipokelewa lugha hugeuka kama nyimbo za singeri tu. "Utatoa hutoi? Nasema Utatoa hutoi?” Hapo ujue msichana anaomba bando la simu kwenye simu.

Kutoka Daddy unaanza kuitwa jina lako halisi la Seleman Wee. Kwenye simu kutoka 'my Love' anaseviwa “Pasua Kichwa." Na ndo hapo sasa tunaambiwa "Wanaume wote ni mbwa."






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags