Diddy Ngoma Ngumu, Mashitaka Kila Kukicha

Diddy Ngoma Ngumu, Mashitaka Kila Kukicha

Wakati mwanamuziki Kanye West akipambana kumrudisha mjini rapa Diddy, mambo yanaendelea kuwa magumu kwa msanii huyo, hii ni baada ya kukumbana na shitaka jingine lililofunguliwa na mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la John Doe.

Mwanamume huyo ambae anafanya shughuli za kuimba na kupiga gitaa mitaa ya nje ya klabu za usiku Los Angeles, anadai kuwa Novemba 2022 mtafuta vipaji wa Diddy alimwalika kwenye sherehe ya rapa huyo.

Aidha aliweka wazi kuwa baada ya kufika nyumbani kwa Diddy alipewa kinywaji huku wakizungumza juu ya matarajio yake ya muziki ila wakati mazungumzo yakiendelea alisifia cheni ya Diddy na ndipo rapa huyo akauliza kama anataka kuona zaidi mkusanyiko wa vito vyake vya thamani.

“Kisha akanipeleka kwenye chumba chake cha faragha, ghafla nilihisi kusinzia na kukosa utulivu na furaha kidogo licha ya kunywa kinywaji kimoja tu,”amesema John Doe.

Doe anadai Diddy alimfanyia vitendo vya unyanyasaji wa kingono huku akimlazimisha kufanya ngono ya mdomo jambo ambalo limekuwa likimtesa kihisia na kiakili.

Hata hivyo Mawakili wa Diddy wameiambia TMZ kuwa mteja wao hatoweza kujibu kila shitaka na madai anayokabiliwa nayo kwani mengine ni ya uwongo na uzushi.

“Kama tulivyosema hapo awali, Bw. Combs hawezi kujibu kila swali jipya la utangazaji, hata kwa kujibu madai ambayo ni ya kipuuzi au ya uwongo unaoonyesha. Bw. Combs na timu yake ya wanasheria wana imani kamili katika ukweli na uadilifu wa mchakato wa mahakama.

Mahakamani, ukweli utatawala: kwamba Bw. Combs hakuwahi kushambulia kingono au kusafirisha mtu yeyote mwanamume au mwanamke, mtu mzima au mdogo,” Wamesema Mawakili wa Diddy.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na Tony Buzbee, ambae ni wakili wa Texas anayewakilisha waathiriwa zaidi ya 120 wanaomshitaki Combs kuhusiana na unyanyasaji wa kingono.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags