Dullah Makabila atoa msimamo kinachoendelea ndoa ya Zaiylissa na Manara

Dullah Makabila atoa msimamo kinachoendelea ndoa ya Zaiylissa na Manara

Mwanamuziki wa Singeli, Dullah Makabila ameiambia Mwananchi kuwa ameumizwa na taarifa zinazodai mwigizaji Zaiylissa ameachana na mumewe Haji Manara.

Dullah ambaye aliwahi kufunga ndoa na Zaiylissa mwaka 2023, amesema angekuwa hajaingia kwenye mahusiano angerudiana na mwigizaji huyo wa Jua Kali.

"Wanaosema nimefurahia ndoa kuvunjika hizo ni stori tu, watu lazima wazungumze hivyo. Ukweli nimejisikia vibaya sana. Kusikia ndoa inavunjika siyo kitu kizuri. Mimi nina mahusiano sasa hivi siwezi kurudiana na Zaiylissa.

"Tena nina mwanamke nampenda sana kiukweli. Halafu mahusiano yenyewe nimeyapata dakika za mwisho lakini ningekuwa sina mahusiano ningerudiana naye," amesema Dullah.

Ndoa ya Dullah na Zai ilidumu kwa muda wa mwezi mmoja tu baada ya kufungwa kwake, kisha wawili hao wakaachana. Ndipo mwigizaji huyo Januari 24, 2024 akaolewa na Haji Manara.

Hata hivyo, kwa Haji ndoa hiyo haikuwa ya kwanza kwani aliwahi kufunga ndoa na wanawake kadhaa akiwemo Rubynah, Rushaynah na Naheedah, huku ndoa yake na Zay ikiwa ya sita kwa Manara kufuatiwa na malezo aliyowahi kutoa mama yake mzazi wakati Haji alipokuwa anafunga ndoa na Rushaynah.

Utakumbuka taarifa ya ndoa ya Zaylissa na Haji kuvunjika imekuja baada ya wawili hao kuanza kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii, huku Zaiylissa akithibitisha kupokea talaka kwenye upande wa jumbe katika chapisho lililowekwa na Juma Lokole.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags