Faida za kufanya mazoezi ya viungo

Faida za kufanya mazoezi ya viungo

Eeebwana eeeh!!!! Unajua kuwa mazoezi ya viungo ni muhimu sana kwa afya yako, ndio ni muhimu na mimi leo nitakujuza zaida kwa nini ni muhimu.

Kabla ya kukueleza faida hizo jua kwamba kuna namna mbalimbali za kufanya mazoezi, unaweza kufanya ya viungo fulani vya mwili wako kama miguu, mikono na mgongo.

Lakini pia kuna mazoezi ambayo ukifanya utakuwa umefanya zoezi lilojumuisha kiungo zaidi ya kimoja mfano; mazoezi ya kukimbia, kuruka kamba na mengineyo.

Licha ya kuwa unaweza kutumia muda kidogo kufanya mazoezi kwa takribani dakika (30-45) kwa siku iwe asubuhi au jioni lakini pia unaweza kupata faida nyingi za kiafya kwa kufanya mazoezi hayo.

Kwa kuwa kuna faida nyingi za kufanya mazoezi basi leo nimeona nikupatie hizi chache kwa manufaa na ufahamu wa afya yako.

Kwanza, ufanyaji wa mazoezi humfanya mtu achangamke na kuwa shupavu pia huboresha ufahamu wako uwezo wa kuelewa na kufikiri mambo katika mazingira yanayokuzunguka.

Pili, mazoezi huboresha uwezo wako wa kuhifadhi kumbukumbu na kukusaidia kupunguza msongo wa mawazo. Ndio ukiwa unafanya mazoezi mara kwa mara huwezi kuwa na msongo wa mawazo.

Tatu, mazoezi huimarisha moyo hivyo hukuepusha na maradhi mengi yatokanayo na mapigo mabaya ya moyo lakini pia humfanya mtu ajiamini.

Nne, mazoezi hupasha mwili joto hivyo husaidia kuzuia baridi na husaidia kuweka sawa kiwango cha cholesterol au mafuta yaliyopo mwilini.

Tano, ufanyaji wa mazoezi hupunguza uwezekano wa mtu kupata ugonjwa wa kisukari, hushusha kupanda kwa shinikizo la damu. (High blood pressure) na hupunguza uwezekano wa mtu kupata baadhi ya maradhi ya saratani.

Sita, mazoezi humsaidia mtu kuondokana na baadhi ya matatizo ya akili, huboresha hamu ya mtu kuweza kula na hupunguza uzito wa ziada wa mwili na kufanya mwili wako kuwa mwepesi.

Mpendwa msomaji hizi ni baadhi ya faida za kufanya mazoezi, lakini pia tukumbuke mazoezi hurefusha maisha kwa kukufanya uwe mwenye afya njema.

Ni vyema ukajiuliza, hivi ni kweli ukifanya mazoezi na kula vyakula bora kunaweza kuboresha maisha yako?

Jibu ni ndiyo mazoezi na vyakula ni dawa pekee ya kutibu au kukuepusha na magonjwa mengi yanayoweza kuzuilika.

Fanya mazoezi kuimarisha afya yako.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags