FAST & FURIOUS toleo la mwisho kuachiwa 2026

FAST & FURIOUS toleo la mwisho kuachiwa 2026

Mwongozaji wa filamu ya ‘Fast & furious 11’, kutoka nchini Marekani # LouisLeterrier amethibitisha kuwa toleo la mwisho la filamu hiyo litaachiwa mwaka 2026  ambapo utayarishaji wake unatarajiwa kuanza mwaka 2025.

Katika mahojiano na Digital Spy, Louis ameeleza kuwa wamesogeza mbele ujio wa filamu hiyo kutokana na mgomo wa mashirika ya uzalishaji filamu nchini humo SAG-AFTRA na WGA mwaka jana  ambao umeathiri sana uzalishaji na utayarishaji wa filamu hiyo.

Katika filamu hiyo ambayo ilitakiwa kutolewa mwendelezo wake mwaka 2025 imeendelea kuwepo kwa nyota waigizaji maarufu kama Jason Momoa, Tyrese Gibson, The Rock na wengine wengi.

Filamu ya mwisho ya ‘Fast & Furious’, itarudisha biashara ya ‘Blockbuster’ katika mji wa Los Angeles nchini humo amabapo ilikuwa ni historia ya kweli ya ‘The Fast and Furious’ iliyotokea mwaka 2001 nchini humo ikimaanisha “Mfungo na Mwenye hasira”

Hivyo mwongozaji huyo aliwataka mashabiki kukaa mkao wa kula kwani yapo mazuri ambayo hawajawahi kuyashuhudia, hata hivyo ameweka wazi kuwa baada ya kukamilisha filamu hiyo kutakuwa na sherehe itakayoandaliwa na waigizaji kwa lengo la kujipongeza kutokana na changamoto walizo kumbana nazo wakati wakiwa wanaandaa filamu hiyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags