Mwenendo wa sherehe ni maamuzi ya muhusika iwaje. Yaani yeye anataka afanye nini ili ipendeze na afurahi.
Waalikwa punguzeni malalamiko na kupangia wahusiaka cha kufanya kwenye sherehe zao. Siyo lazima wafanye kama mnavyotaka nyie.
Usione walipendeza kwenye sherehe ya Hamisa na Aziz Ki. Lakini walinuna balaa, baada ya kukuta maua ni mengi kuliko msosi.
Sasa je, kama Hamisa na bebi wake wanapenda maua nyie mnanuna nini. Huko mitandaoni wanalilia vinywaji na vyakula, wakati hawakutoa mchango hata mia mbovu.
Shida watu wengi huku mitaani, wameweka mbele kwenda kula kwenye sherehe za watu na siyo kuonesha sapoti kwa muhusika. Eti wanasema sherehe ni chakula na vinywaji. Jamani punguzeni lawama.

Leave a Reply