Feisal apewa masharti matatu Yanga

Feisal apewa masharti matatu Yanga

Rais wa Yanga Mhandisi, Hersi Said amesema kuna machagua matatu ya kiungo Feisal Salum maarufu kama Fei Toto ya kuendelea kusalia Yanga kuendelea kutumikia mkataba au kuondoka klabuni hapo.

Hersi amesema hayo leo Jumatano Mei 24, 2023 alipokuwa akifanya mahojiano na moja ya chombo cha habari ametaja mambo hayo ikiwa ni; Arudi kutumikia mkataba wake, Kama kuna tatizo la maslahi Yanga wapo tayari kumsikiliza na mwisho akitaja timu inayomtaka iende mezani.

“Sitaki kwenda mbali ila mimi naamini kuna kitu nyuma ya Feisal kinachomsukuma kufanya haya, kuvunja mkataba inaruhusiwa lakini pale ambapo pande zote mbili mnapokuwa mmeshindwa kufikia makubaliano, kitu ambacho kwa Feisal hakipo kwasababu Yanga tumetekeleza yote ambayo anapaswa kutekelezewa Feisal hivyo mamlaka zikamtaka Feisal kuendelea na mkataba wake,” amesema Hersi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags