Filamu ya Usher kuanza kuoneshwa Septemba 12

Filamu ya Usher kuanza kuoneshwa Septemba 12

Mkali wa R&B kutoka Marekani Usher Raymond ametangaza kuachia filamu ya matamasha yake nane aliyoyafanya jijini Paris,Ufaransa mwaka jana.

Usher ameyasema hayo katika taarifa yake na vyombo vya habari kwa kueleza kuwa ameamua kutoa filamu hiyo hasa kwa wale ambao hawakuhudhuria ili kufanikisha kutizama tukio zima.

“Paris ilikuwa tukio maalum kwangu kama mburudishaji na kwa mashabiki wangu, hii itakuwa mahususi kwa wale ambao hawakuweza kuhudhuria ili kushuhudia ilivyokuwa, pia kwa waliokuwepo kuweza kutazama onyesho kwa ukaribu”



Filamu hiyo ya Usher iliyopewa jina la ‘Usher: Rendezvous In Paris’ inatarajiwa kuoneshwa katika zaidi ya kumbi za sinema 2,000 duniani kote kuanzia Septemba 12-15 mwaka huu huku ngoma kama ‘My Boo’, ‘Love In This Club’ na ‘Yeah!’ zitajumuishwa katika filamu hiyo pamoja na kuangalia maisha ya msanii huyo nyuma ya jukwaa.

‘Usher: Rendezvous In Paris’ imeongozwa na mtayarishaji filamu Anthony Mandler, ambaye pia ameshafanya kazi na Taylor Swift pamoja na Beyoncé.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags