Hali bado tete kwa mchezaji Martinez

Hali bado tete kwa mchezaji Martinez

Beki wa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited, #LisandroMartinez inadaiwa atakuwa nje ya uwanja kwa miezi mitatu kutokana na jeraha la mguu wa kulia.

Kwa mujibu wa taarifa inadaiwa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina alifanyiwa upasuaji wa mguu ambao umekuwa ukimuuma kwa muda, alikumbana na jeraha hilo kwa mara ya kwanza Aprili, mwaka huu na alikuwa nje kwa wiki 11.

Aidha raia huyo wa Argentina alirejea wakati wa maandalizi ya msimu mpya na alicheza ‘mechi’ nne za ufunguzi wa ‘Ligi’ kuu ya England.

Lakini alijitonesha tena wakati wa ‘mechi’ dhidi ya Arsenal na akatolewa nje kulingana na vipimo vilivyotoka ‘wiki’ hii vinaonyesha kuwa beki huyo bado hajapona vizuri na kunauwezekano wa kufanyiwa upasuaji haraka iwezekanavyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags