Jay-Z Amshitaki Buzbee Kwa Kumchafua

Jay-Z Amshitaki Buzbee Kwa Kumchafua

Baada rapa na mfanyabiashara kutoka Marekani Jay-Z kushinda kesi ya unyanyasaji wa kingono iliyofunguliwa na mwanadada Jane Doe Disemba 9, 2024. rapa huyo ameripotiwa kumshitaki wakili wa kesi hiyo Tony Buzbee kwa madai ya kumchafua huku akihataji kulipwa fidia zaidi ya Sh 51 bilion.

Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa Mahakamani na JayZ zimeeleza kuwa kesi hiyo imemchafulia jina lake kwa kiasi kikubwa na kupelekea apoteza mikataba na makampuni makubwa ambayo yalipanga kumlipa kiasi cha dola milioni 20 ikiwa ni zaidi ya Sh 51 bilioni.

“Nilihisi kwamba Buzbee alikuwa akiniwekea Silaha (bunduki) kichwani, kwamba ama nikubali matakwa yake au nivumilie Hasara Ya Kifedha, madai hayo yameleta maumivu makubwa kwa familia yangu. Mke wangu na mimi tutalazimika kukaa na watoto wetu chini... na kuelezea ukatili na tamaa ya watu,” amesema Jay Z

Utakumbuka kuwa wakili Buzbee ambae pia anasimamia kesi zaidi ya watu 120 wanaomshitaki Diddy, alimfungulia Jay Z kesi ya unyanyasaji wa kingono akimtuhumu rapa huyo kufanya ubakaji kwa binti aliefahamika kwa jina bandia la Jane Doe mwenye miaka 13 mwaka 2000, tukio ambalo lilimuhusisha pia rapa Diddy.

Wanasheria wa Jay-Z walikanusha madai hayo na kuombwa ya tupiliwe mbali lakini pia kwa upande wa rapa huyo anasema hayana ukweli na yameathiri vibaya jina lake pamoja na maslahi yake ya kibiashara. Mpaka sasa Tony Buzbee hajatoa tamko rasmi kuhusu tuhuma hizi. Kesi hii inatarajiwa kufuatiliwa kwa karibu na wadau wa sheria.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags