Je wajua binti akisuka hivi yupo kwenye balehe

Je wajua binti akisuka hivi yupo kwenye balehe

Tunajua unajua lakini tunakujuza zaidi, wakati Bongo baadhi ya vijana wakijitahidi kuficha hatua za ukuaji (balehe), lakini kwa tamaduni za Kusini mwa Angola hakuna siri kwenye hilo kwani kila msichana atakaye balehe atasukwa mtindo huo wa nywele.

Wasichana wa kabila la Ovankhumbi wanapokaribia au wakiwa wanaanza balehe wanasukwa nywele zinazofumwa kwa ustadi mkubwa unaotumia uzi asili ambapo msuko huo unaashiria utambulisho wao wa kitamaduni na safari yao ya kuingia utu uzima.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali unaeleza kuwa mtindo huu ulianzishwa miaka mingi iliyopita huku ukiendelea kutumika na kabila hilo kwa ajiri ya kuenzi/kurithi tamaduni za kale za Kusini mwa Angola.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags