Ibrah Athibitisha Kufunga Ndoa

Ibrah Athibitisha Kufunga Ndoa

Baada ya kuwepo kwa tetesi katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Ibrah amefunga ndoa na msichana kutoka Burundi, hatimae msanii huyo amethibitisha hilo.

Akizungumzana moja ya chombo cha habari kwa njia ya simu ameeleza kuwa kwasasa yupo Burundi kwa ajili ya shughuli za muziki na sio kwamba ameenda kufunga ndoa kama ambavyo wadau mbalimbali walivyokuwa wakieleza.

“Burundi nimeitwa nimekuja kusalimia wazazi, mimi nishaoa na nimeshazungumza hilo au mlikuwa mnachukulia ni kiki amna kwasasa mimi nina mke.

Nimekuja kusalimia pia kulikuwa kunashow kadhaa lakini soon narudi nyumbani nakuja kumalizana na vimeo kadhaa, nimekuja kuona wakwe wameniambia siwezi kuoa harafu ikwa hujaja kuona wazee,”amesema Ibrah

Ikumbukwe msanii huyo ameondoka Bongo tangu amalizane na lebo yake ya Konde Gang inayomilikiwa na Harmonize miezi michache iliyopita ambapo kwasasa akiwa kama msanii huru anatamba na ngoma ya ‘Asante’ aliyoiachia wiki mbili zilizopita.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags