Hawajaimba Lakini Wamepata Umaarufu

Hawajaimba Lakini Wamepata Umaarufu

Muziki ukiwa kazi kama kazi nyingine umeweza kuwa na nguvu ya kubadilisha maisha ya watu. Sio tu wasanii bali hata watu ambao hupata fursa ya kucheza nafasi mbalimbali kwenye nyimbo za wanamuziki.

Kuna baadhi ya nyimbo zimekuwa kubwa na kuibua vipaji vya watu wengine pia kuwakuza kisanaa huku wakipata mafanikio. Japo nyimbo hizo hawajaimba lakini wameshiriki kama video vixen, video king, ama dansa. Hizi ni baadhi.

Aviola, huu ni wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Mbosso unaopatika kwenye Ep yake Room Number 3. Ikiwa kama moja ya ngoma iliyofanya vizuri, lakini imeleta staa mpya ambaye ni Bonge la Dada. Sio tu umaarufu lakini pia imembadilishia maisha na kutambulika kama mmoja wa densa anayefanya vizuri kwa sasa.

Bonge la Dada sio jina la wimbo lakini kwenye sehemu ya kiitikio ndiyo Mbosso anasikika akiimba Bonge la Dada X 8. Wimbo huo umeweza kumleta Bonge la Dada 'Queen Fraison' ambaye umaarufu wake aliupata wakati Mbosso kuzindua Ep hiyo Juni 12, 2025.

Zuwena, wimbo wa nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ambao ulitoka 2023 uliweza kumuibua na kumpa umaarufu mwanamke aliyeigiza kama Video Vixen .Na mpaka sasa anatumia na kutambulika kama Zuwena jina kutoka kwenye wimbo huo wa Diamond. Zuwena ameweza kujiongeza na kuingia kwenye sanaa rasmi ya Uigizaji.

Masogange, moja kati ya ngoma bora za muda wote kutoka kwa mkali wa Bongo Fleva, Belle 9 ambapo mafanikio yake sio tu yalikuwa kwenye wimbo huo, bali ulifanikiwa kuzalisha staa mpya na mmoja kati ya wanamapinduzi kwenye sekta ya Video Vixen, marehemu Agnes Masogange. Licha ya kutokuwa hai lakini bado anaendelea kuishi kwenye mioyo ya mashabiki wa muziki nchini.

Agnes Masogange alifariki dunia Ijumaa, Aprili 20, 2021, majira ya 4.00 jioni. kwa mujibu wa aliyekuwa mwanasheria wa marehemu Masogange, Roben Simwanza alisema alikuwa akisumbuliwa na nimonia na alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge katika Manispaa ya Kinondoni.

Amelowa, wimbo wa msanii wa Bongo Fleva, Harmonize uliyotoka 2022. Wimbo huo umempa umaarufu video vixen aliyecheza Sophia Amelowa ambaye baada ya kufanya kazi nzuri kwenye video hiyo akatambulika kwa ukubwa zaidi.

Aidha, wimbo wa msanii wa rapu nchini Rapcha ambao uliachiwa rasmi 2021 umeweza kuzalisha staa mwingine aliyecheza kama Video Vixen kwenye wimbo huo ambaye hakuhusika kutia neno hata moja katika wimbo huo, Eva Nchidange Lissa kutokana na wimbo huo alitambulika vizuri na kumpatia umaarufu zaidi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags