Mtandao wa kuuza na kusikiliza muziki Spotify umetoa orodha ya wasanii na nyimbo zinazosikilizwa zaidi nje ya nchi katika muhula wa nusu mwaka wa 2025.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo wimbo namba moja unaosikilizwa sana nje ya nchi ni wa Jux ‘God Design’ wimbo ambao aliyomshirikisha rapa Phyno kutoka Nigeria. Ukiachana na wimbo huo mastaa wengine wanaokimbiza ni pamoja na Diamond Platnumz na Harmonize.
Kolabo hiyo na Phyno, imekuwa hatua ya mafanikio kimataifa kwa msanii Jux ambaye amekuwa akisifika kutokana na uimbaji wake wa R&B ambapo kwa mujibu wa ripoti hiyo msanii huyo ameonesha uwezo mkubwa ambao unaendelea kuusukuma muziki wa Tanzania Kimataifa.
Japo God Design umeshika chati, Diamond Platnumz ameendelea kuwa msanii kutoka Tanzania anayeongoza kusikilizwa nje ya nchi, nyota huyo wa Bongo Fleva ametajwa kukonga nyonyo za mashabiki kufuatia na nyimbo zake zenye radha tofauti.
Data hizo kutoka Spotify zinaonesha muziki wa Tanzania unaendelea kuongeza wasikilizaji zaidi duniani ikiwemo nyimbo za Jay Melody (Turudiane, Nitampata Wapi, Nazama), Jux (YOU, CELEBRATION, MY SHAYLA), Harmonize (Finally, Furaha, Pere), ni kati ya nyimbo nyingi zinazoendelea kusikilizwa zaidi nje ya mipaka ya Tanzania.
Aidha mwanamuziki Jay Melody ametajwa kuwa msanii pekee anayewavutia mashabiki mbalimbali kutokana na sauti yake pamoja na mistari yake inayoelezea stori akijizolea umaarufu kuanzia Nairobi hadi Berlin.
Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti hiyo moja ya sababu zinazochangia muziki wa Tanzania kusikilizwa zaidi nje ni wasanii wa Bongo kushirikiana na wasanii kutoka nje, kolabo kama ‘Katam’ ya Diamond aliyomshirikisha Bien pamona na ‘Alone’ ya Rayvanny aliyomshirikisha rapa kutoka Uingereza, Headie One.
Mbali na hayo inaelezwa kuwa kwa muda mrefu, Nigeria na Afrika Kusini zimekuwa zikitawala jukwaa la muziki barani Afrika lakini data hizo zinaonesha kuwa Tanzania inaopanda kwa kasi hivyo basi kwasasa muziki wa Bongo umekuwa na ushindani mkubwa na nchi hizo mbili katika majukwaa ya kimataifa.

Leave a Reply