Kwa kawaida watu wengi wanafahamu kuwa nyanya ni kiungo ambacho kinatumika katika kuungia mboga lakini pia ni tunda ambalo baadhi ya watu hupendelea kulila bila kufahamu unaweza kutengenezea juice na ikakusaidia kiafya.
Nyanya mbichi ni chanzo cha Vitamin A, Vitamin K, Vitamin B1, B2, B3, B5 na B6, pamoja na madini kama magneziam (magnesium), chuma (iron) na fosforas (phosphorus).
Ukiachilia mbali kufanikisha kutoa chakula kizuri jikoni lakini pia ni moja ya kiungo/tunda ambalo linafaida mbalimbali zikiwemo kusaidia katika uponyaji wa vidonda na majera na hii ni kutokana na Vitamin K iliyomo ndani yake.
Lakini pia inaweza kusaidia kupunguza dalili za kukoma hedhi. Utafiti wa mwaka 2015 uliofanywa na jarida la lishe, Nutrition Journal uligundua kuwa unywaji wa sharobati (juice) ya nyanya ulionekana kusaidia kuboresha baadhi ya dalili za kukoma hedhi kama vile wasiwasi na mapigo ya moyo.
Baada ya kufahamu hayo fahamu namna ya kutengeneza juice ya nyanya kwa ajili ya biashara.
Mahitaji
- Nyanya kubwa 3-5
- Chumvi nusu kijiko kidogo
- Sukari kijiko kimoja
- Tangawizi, hiriki, passion au vanilla (sio lazima uweke vyote unaweza kutumia kimoja kwa ajili ya kushangamsha juice yako)
- Maji nusu lita
Jinsi ya kuandaaa
- Osha nyanya zako vizuri na uanze kuzikatakata vipate kisha weka katika bakuli safi
- Baada ya hapo chukua viungo vingine kati ya passion, hiriki au tangawizi changanya katika bakuli lako la kwenye nyanya.
- Ukishamaliza hapo tia kwenye brenda mchanganyiko wako na uanze kuusaga mpaka pale utakapolainika vizuri.
- Kisha chuja juice yako na uongeze chumvi kiasi, sukari na ndimu au unaweza kutumia kimoja wao. Mpaka kufikia hapo unaweza kuweka juice yako katika friji na tayari kwa ajili ya kunywewa.
Leave a Reply