Mkali wa Hip Hop kutoka Canada Drake, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuonekana amefuta tattoo ya mchezaji nyota wa mpira wa kikapu, LeBron James, aliyokuwa ameichora kwenye mkono wake wa kushoto.
Tukio hilo limeibua maswali mengi kwa mashabiki na wachambuzi wa burudani, wakijiuliza kama wawili hao ambao pia ni marafiki wa muda mrefu kuwa wamegombana.
Aidha kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vinaeleza kuwa Drake ameamua kufuta tattoo hiyo baada ya Lebron kuhudhuria katika onyesho la Kendrick Lamar ‘Pop Out’ jambo ambalo lilimkera rapa huyo kwani anabifu na Lamar.
Drake, ameonesha mara kadhaa mapenzi yake kwa LeBron kupitia mistari ya nyimbo na hata uwepo wake katika mechi mbalimbali za NBA, alichora tattoo hiyo kama ishara ya heshima na kuvutiwa na mafanikio ya nyota huyo wa Los Angeles Lakers.
Ikumbukwe Drake alichora tattoo hiyo mwaka 2018, ikichorwa na mchoraji maarufu wa wasanii Marekani Inal Bersekov.

Leave a Reply