Wakiwa na miezi sita tu tangu kuweka wazi uhusiano wao, Jux na Priscilla Ojo ‘Hadiza’ wamekuwa wakitoa somo zuri kwa mashabiki na wadau wa Bongo kuhusiana na maana nzuri ya mahusiano kwani wamekuwa wakifanya mambo ambayo kwa kapo za bongo wahajawahi kuyafanya.
Achana na ile ya Nandy na Billnass, au ile kongwe kabisa ya Aika na Nahreel au pezi jipya kati ya Aziz Ki na Hamisa Mobetto ukiwakutanisha wote unaweza kusema vipo vitu vya kujifunza kutoka kwa wawili hao ambao wameiteka mitandao ya kijamii ya Tanzania na Nigeria kupitia mapenzi yao.
Uhusiano wao ulidaiwa kuanza mwishoni mwa 2023 lakini waliweka wazi uhusiano wao katika mitandao ya kijamii Agosti 2024 huku mambo yakishamiri zaidi baada ya Jux kwenda ukweni Nigeria ambapo alipokelewa kwa shangwe na mkwe wake ambaye ni mwigizaji mkongwe Nigeria Iyabo Ojo.
Hatimaye, Februari 7, 2025, wawili hao walithibitisha mapenzi yao kuwa ya kweli ambapo walifunga ndoa ya kiislam, ikawa moja ya harusi kubwa zilizovuta hisia za mashabiki kutoka Tanzania, Nigeria, na kwingineko huku ndoa hiyo ikionekana kuwa muunganiko mzuri kwa mataifa hayo.
Japo kumekuwa na komenti baadhi katika mitandao ya kijamii zidai kuwa ‘Wataachana Tuu’ lakini wawili hao wameendelea kuwakera watesi wao ambapo Februari 12, 2025 Jux alifanikiwa kumvesha pete ya pili mpenzi wake huyo mbele ya familia yake.
“Baby, nakuchumbia kwa mara ya pili, lakini safari hii mbele ya familia yako na marafiki zako wa karibu, na pete yenye ukubwa mara mbili, Nakupenda kwa moyo wangu wote, na siwezi kusubiri kutumia maisha yangu yote pamoja na wewe, mpenzi wangu,” ameandika Jux katika ukurasa wake wa Instagram.
Mbali na hilo lakini pia siku ya jana Februari 13,2025 wawili walifanya sherehe nyingine ambayo ilihudhuriwa na familia na ndugu wa karibu, huku kukiwa na tetesi kuwa wawili hao jana ndio walifunga ndoa ya serikali.

Leave a Reply