Kaeda aishukuru TFF kwa tuzo, aahidi kuishangilia Yanga popote

Kaeda aishukuru TFF kwa tuzo, aahidi kuishangilia Yanga popote

Nyota wa zamani wa Yanga Princess ambaye kwa sasa anakipiga UTAH ya Marekani, Kaeda Wilson maarufu Mzungu, amesema ataendelea kuishangilia na kuishabiki timu hiyo hata kama yuko mbali.

Kiungo huyo raia wa Marekani, alijiunga na Yanga Princess msimu uliopita akitokea 7 Elite Akademi ya nchini kwao ambapo alifanikiwa kufunga mabao manne katika Ligi Kuu Soka Wanawake wakati timu yake ikimaliza nafasi ya tatu.

Mbali na hilo, nyota huyo kwenye usiku wa Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alitajwa katika kikosi bora cha Ligi Kuu Soka Wanawake 2023-2024 ambapo tuzo yake ilipokewa na mwakilishi wake kutokana na yeye kutokuwepo eneo la tukio.

Kaeda amepiga picha akiwa na tuzo hiyo na kuiweka katika akaunti yake ya Mtandao wa Instagram ambapo katika ujumbe wake amewashukuru mashabiki pamoja na timu ya Yanga Princess ambayo ameahidi kuishabikia hata kama yupo mbali ku.

"Huu ni ujumbe kwa TFF na wapiga kura kuhusu tuzo hii, ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa TFF na wapiga kura kwa tuzo hii ya kipekee, nilifurahia sana kucheza nchini Tanzania na nilipata baadhi ya uzoefu bora zaidi maishani mwangu.

"Hivi sasa nipo Utah nikichezea Utah State University na naendelea kujifunza na kukuwa kama mchezaji. Ingawa nipo mbali, nitakuwa nikifuatilia Ligi Kuu ya Tanzania na nitakuwa nikishangilia Yanga popote nilipo.

"Nitaendelea pia kuwatakia mema wachezaji wenzangu wa zamani na dada zangu, popote watakapokuwa wakicheza, kwa mashabiki wa Yanga kila la heri na Daima Mbele Nyuma Mwiko," aliandika kiungo huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags