Kama mpenzi wako au Mumeo hakuridhishi mfungukie

Kama mpenzi wako au Mumeo hakuridhishi mfungukie

Ooooohooooooh! It’s another Monday jamani kama kawaida yetu kwenye ile segment ya mahusiano yani huwa hatufichi kitu waswahili wanasema mambo yote waaaah.

Sasa leo bwana tumekuja na suluhisho linalo wakumba wadada wengi lakini wanaogopa kuzungumaza, skiliza nikawambie mwanangu sana kama usipo mfungukia mpenzi wako nani atamfungukia, jamani eeeeh kama mpenzi wako, mumeo hakuridhishi mfungukie bwana kwanini uvunge.


Kufikia kilele cha Mlima Kilimanjaro au kufika mshindo, kuridhishana mnapokuwa faragha, penzi ni tamu kama ukimpata anayeyajua mapenzi, kisha mkaridhiana, mkaele­wana hakika mtayafurahia mapenzi yenu.
Wanaume wengi huweza kufurahia tendo la ndoa wa­napokuwa na wenza wao, kuliko wanawake, wanaume wanaweza kufikia mshindo kwa haraka zaidi kuliko wanawake.


Wakati idadi kubwa ya wanaume ikiongoza kwa kufikia mshindo, wanawake wengi zaidi hushindwa kufurahia tendo hilo na kuishia hewani.

Kama nilivyosema awali, mapenzi ni kuridhiana, kuelewana, kukubaliana sasa inapotokea mko faragha halafu mmoja wapo anafurahia na mwingine anaishia kunukia shombo ya mchezo si sawa.
Na mbaya zaidi anayeishia kugugumia kwa maumivu anachukuliwa poa, eti alishazoea.

 Hili ni tatizo tena kubwa ambalo linaweza kusabisha usaliti katika uhusiano wenu.
Tatizo hili linaweza kuku­fanya uanze kuwaza namna ya kuchepuka ili kutafuta tamu ya penzi au wewe mwanaume unaweza kuwa chanzo cha mwanamke kukudharau na kutokukupenda.

Baadhi ya Sababu sinazo mfanya mwanamke asimwambie mumewe ukweli kuhusu kuto kuridhika


kuonekana malaya
Baadhi ya wanawake wanashindwa kuwaambia ukweli wapenzi wao pindi am­bapo hawafurahii tendo la ndoa kwa kuhisi anaweza kuonekana ni malaya ali­yekubuhu au ni mwanam­ke anayependa sana ngono kuliko kitu kingine.
Kwa mantiki hiyo, mwan­amke huamua kupotezea na kubaki akigugumia kwenye mtima wake. Jambo am­balo ni hatari kwa uhusiano wake.


kuonekana hana adabu
Wanawake wengine huona tu aibu kuzungumzia suala la faragha na mwen­za wake kwa kuamini kuwa halipaswi kuzungumzwa. Anaona ni bora kufa na tai yake shingoni kuliko kusema ukweli.
Wewe mwanam­ke unayeona aibu kuzungumza na mwenza wako kuhusu ki­nachokusi­bu hasa mnapokuwa faragha unakosea kwa kuwa inawezeka­na mwenza wako hajagund­ua tatizo
hilo, yeye anahisi ni kidume cha mbegu kwa sababu anakufurahisha kumbe uk­weli hujawahi kufurahia.

mwanaume kuwa mkorofi/ mwanaume kutomskiliza mwenza wake
Wakati mwingine mwa­namke anaweza kuhofia kumwambia mwanaume kwa sababu ya tabia au ukorofi alionao.
Pengine huwa hasikili­zi ushauri na maoni yake hivyo anaona hata jam­bo hilo akikuambia itakuwa yaley­ale tu.
Kwa tabia hiyo ya kujiona yeye ni kila kitu bila kumpa nafasi mwenza wake, hukosa mambo mengi na mwisho wake hukaribisha michepuko kwenye penzi au ndoa.

haya haya wanangu wa mwananchi scoop embu dondosha komenti yako hapo chini kutuambia ni sababu zipi nyingine zinazomfanya mwanamke asifunguke ukweli.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags