Kanye West Auanza Mwaka Vizuri

Kanye West Auanza Mwaka Vizuri

Mwanamuziki wa Marekani, Kanye West ameuanza mwaka vizuri kwa kupata maokoto ya kutosha, hii ni baada ya kuripotiwa kuwa mwanamuziki tajiri zaidi duniani kwa mwaka 2025.

Kwa mujibu wa ‘Erin Venture Service, imeeleza kuwa msanii huyo ameongeza mpunga wa kutosha Januari hii na kupelekea utajiri wake kupanda ambapo mpaka sasa anakadiriwa kufikia dola bilioni 2.77.

Ongezeko la fedha hizo zinadaiwa kutokana na mafanikio yake ya kimuziki pamoja na chapa yake ya YEEZY inayoendelea kufanya vizuri kila siku huku akiwa na mpango wa kupanua chapa hiyo kwa kuzindua mavazi ya wanawake ya YEEZY.

Utakumbuka kuwa mapema mwezi huu Kanye West alionesha ukubwa wake katika biashara kufuatiwa na mauzo aliyoyapata kwa kuingiza dola milioni 3 kupitia bidhaa hizo ndani ya masaa 30.

Mauzo haya yalitokana na uzinduzi wa hivi karibuni wa bidhaa na mitindo mipya ya Yeezy, ambayo ilitoa bidhaa kama mavazi na viatu kama toleo maalumu kwa mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags