Baada ya Kendrick Lamar kuzikomba tuzo 5 za Grammy wiki iliyopita, usiku wa kuamkia leo Februari 10,2025 alitumbuiza kwenye 'Half Time Show ya Super Bowl ya 59', iliyofanyika huko New Orleans Louisiana katika Uwanja wa Caesar Super Dome.
Show hiyo ilipangiliwa kwa namna ya kutoa stori fulani, kama Kendrick alivyoahidi kwenye mahojiano aliyofanya na Apple Music siku chache kabla ya shoo hiyo.
Kendrick alitumbuiza ngoma zake kama Squable Up, Humble, TV Off, Not Like Us, All Stars na nyingine nyingi. Lakini pia shoo hiyo ilichukua nafasi ya kipekee kwani aliamua kumtumia muigizaji Samuel Jackson 'Anko Sam' ambaye alikuwa kama host anayempa link za kutoka kwenye wimbo mmoja kwenda mwingine.
Hata hivyo, katika shoo hiyo iliyohudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Rais Donald Trump na amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani kuhudhuria mashindano hayo. Mbali na Trump pia alikuwepi Jay Z na familia yake mwanasoka Lionel Messi na mastaa wengine.
Aidha ubora wa shoo aliyofanya Kendrick umemfanya mwanamuziki Chris Brown kushindwa kuzuia hisia zake. Muda mchache baada ya Kendrick kushuka kwenye jukwaa Chris aliachia ujumbe kwenye Instagram story yake akisema,
“Wow Dot” na kisha kuweka emoji ya moto akionesha kukubali alichokifanya rapa huyo wa Compton California.
Super Bowl ambayo ipo chini ya Apple Music ni show fupi ambayo hufanywa kwa takribani dakika 13 za muda wa mapumziko kwenye fainali za mashindano ya mchezo huo kila mwaka.
Mashindano hayo hutoa nafasi kwa wasanii kuwa kinara kwa mwaka husika ambapo 2025, Kendrick iliangukia mikononi mwake.
Kendrick anakuwa sio msanii wa kwanza kutumbuiza kwenye jukwaa hilo utakumbuka 2024 alifanya Usher Raymond, 2023 Rihanna 2022 wengine ni Dr.Dre, Snoop Dogg, Eminem, Mary J, 50 Cent lakini pia Kendrick Lamar alipata nafasi ya kutumbuiza mwaka huo.

Leave a Reply