Kesi Ya Salman Khan Kuhusu Uwindaji Haramu Yapamba Moto

Kesi Ya Salman Khan Kuhusu Uwindaji Haramu Yapamba Moto

Kesi ya mwigizaji wa Bollywood, Salman Khan inazidi kupamba moto ambapo inatarajiwa kurudishwa tena Mahakama kuu ya Rajasthan, Septemba 22,2025 kwa ajili ya kusikiliza rufaa dhidi ya hukumu iliyotajwa mwaka 2018.

Utakumbuka kuwa Khan alifunguliwa kesi mwaka 1998 ya uwindaji haramu wa swala mweusi tukio ambalo lilitokea wakati wa utengenezaji wa filamu ya ‘Hum Saath Saath Hain’ katika kijiji cha Kankani, wilayani Jodhpur. Ambapo mwaka 2018 alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.



Siku ya Jumatano mahakama hiyo ilieleza kuwa mwezi September pia itasikiliza ombo la rufaa ya kuachiwa huru kwa washitaki wenzake na Khan ambao ni Ali Khan, Tabu, Sonali Bendre, Neelam na Dushyant Singh, kesi hiyo inayotarajiwa kusikilizwa na jaji Manoj Kumar Garg.

Aidha wakili wa upande wa mashtaka, Mahipal Bishnoi, alisema kuwa wanasheria wa Salman Khan waliomba kesi hiyo ihamishiwe Mahakama Kuu ili isikilizwe kwa pamoja na ombi la kukata rufaa kwa washtakiwa wengine, lakini mchakato huo hautowezekana kutokana na sababu za kiufundi.

Filamu hiyo ya ‘Hum Saath-Saath Hain’ ambayo imesababisha msala kwa Khan ilitoka rasmi Novemba 5,1999 filamu ambayo iliongozwa na Sooraj R. Barjatya na kuigizwa na mastaa wakubwa wa Bollywood akiwemo Salman Khan, Saif Ali Khan, Tabu, Sonali Bendre, Neelam na wengine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags