Ikiwa ni wiki tatu mfululizo tangu kuanza kusikilizwa kesi ya rapa kutoka Marekani Sean "Diddy" Combs, na sasa msaidizi mwingine wa Diddy ametoa ushahidi akidai kuwa alinyanyaswa kingono mara kadhaa na msanii huyo.
Wakati alipokuwa akitoa ushahidi katika mahakama ya Manhattan, jana Mei 29, 2025 msaidizi wa zamani wa Diddy aliyefahamika kwa jina la bandia ‘Mia’ alieleza kuwa alipata nyanyasaji wa kingono na kimwili alipokuwa akifanyakazi kwa msanii huyo mwaka 2009 hadi 2017.
Mia alieleza kuwa Combs alimbaka mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na tukio la kumbaka kitandani kwake wakati wa sherehe ya siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 40.
Aidha Mia aliendelea kwa kudai kuwa Diddy alimpiga, kumtupa ukutani na kumtishia mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kumshambulia kwa kutumia vitu mbalimbali kama bakuli.
Akizungumza kuhusiana na vitendo alivyokuwa akifanyiwa mpenzi wa zamani wa Diddy, Cassie Ventura mfanyakazi huyo ameeleza kuwa alikuwa akihusika kufanya usafi kwenye vyumba vya hoteli na kukuta damu ya hedhi, vioo kuvunjika pamoja na chupa za mafuta zilizotapakaa chumba kizima.
Combs, mwenye umri wa miaka 55, atakabiliwa na kifungo cha maisha gerezani endapo atapatikana na hatia katika mashtaka ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, uhalifu wa kupanga na mashtaka mengine. Lakini rapa huyo amekana mashtaka yote dhidi yake.
Utakumbuka Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn.

Leave a Reply