Kifahamu kijiji chenye uhaba wa wanaume

Kifahamu kijiji chenye uhaba wa wanaume

Na Asma Hamis

Kuishi kwingi ndiyo kuona mengi msemo huu wa wahenga unajionesha katika kijiji cha Noiva do Cordeiro kilichopo nchini Brazil chenye watu 600.

Kijiji hicho kinaripotiwa kuwa na uhaba wa wanaume huku wanawake waishi huko wakihitaji wanaume zaidi ili kuongeza idadi yao.

Kawaida kwenye kijiji hicho wanakaribishwa wageni kwa sharti la kuzingatia lazima wawe wanaume kwa lengo la kuoa na kuanzisha uhusiano na wanawake wapatikanao hapo.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘The Week’ wanaume wote wa kijiji hicho wanatumia muda mwingi kwenda kutafuta maisha mijini huku wakiwaacha wanawake wao wakiwa wenyewe kwa takribani wiki mbili hadi mwezi.

“Sijambusu mwanaume kwa muda mrefu na sote tunaota ndoto za kupendwa na kuolewa lakini hazitimii, tunapenda kuishi hapa na hatutaki kuondoka kijijini kutafuta waume,” alisema mwanamke mmoja

Kijiji hicho ambacho kimejitenga kinakadiriwa kuwa na umbali mrefu kutokea mjini, kilianzishwa mwaka 1891 na mwanamke aitwaye aitwaye Maria Senhorinha de Lima huku jina la kijiji hicho likiwa na maana ‘Bibi Harusi wa mwanakondoo’.

Aidha mkazi mwingine wa kijiji hicho aliyejitambulisha kwa jina la Rosalee Fernandes (49) alieleza kuwa wanaume wanapoondoka huwalazimu hutatua matatizo ki kike.

“Panapokuwa na matatizo au migogoro, tunatatua kwa njia ya kike, tukijaribu kupata mwafaka badala ya mgongano. Tunapenda kuwajua wanaume ambao wako tayari kuacha maisha yao na kuwa sehemu yetu lakini kwanza wanahitaji kukubali kufuata tunavyosema na kuishi kulingana na sheria zetu,” alisema Fernandes






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags