Konde Boy, mkopo hulipwa na mkopo

Konde Boy, mkopo hulipwa na mkopo

Chukua huku weka pale, chukua kule lipa hapa. Cha msingi wakopwaji wasijuane. Yes! Konde anadaiwa na benki kiasi cha kupelekana kwa pilato. Zaidi ya milioni mia, ni sehemu ya mkopo wa milioni mia tatu aliochukua. Ni sifa za ‘bizinesi mani’ wala siyo aibu na ajabu.

Huwezi tajirika bila kukopo. Ila unaweza kufilisika kwa mikopo. Konde kashindwa kuchanga karata vizuri mpaka Pilato kamuamuru alipe. Dunia nzima matajiri wakubwa ni wakopaji. Kuacha ‘ishu’ ifike Mahakamani Divisheni ya Biashara, ni kosa la kiufundi.

Pengine ‘menejimenti’ ya mchizi inahitaji akili ya juu yake. Kuongozwa na akili ya ziada. Kifupi ni picha mbaya kwa taasisi zingine za mikopo. Milioni mia moja ni pesa ndogo kwa Konde. Alikuwa na sifa ndiyo maana benki wakatoa mzigo mrefu. Na yeye kalipa parefu hadi kubaki milioni mia katika tatu.
Kwanini kaacha korido za ‘upilatoni’ ndo ziamue? Shida iko hapo! ‘neksi taimu misteki’ ndogo kama hizi ni za kuzimaliza kinyamwezi gizani kwa faida ya kesho.

Pamoja na yote kuna hasi na chanya. Hasi ni uaminifu kwa taasisi zingine. Na chanya ni jamii kujua biashara ya muziki ni dhamana tosha.

Achana na ‘kupushi’ ndinga na mijengo ya maana. Umejiuliza kiasi cha milioni mia tatu kukopeshwa msanii yule? Benki ilimuaminije? Hapo ndipo utajua muziki ni biashara kubwa. Kiba na Mondi wanashindana kumiliki media. Kondi Boy na madeni yake ya benki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags