Koti la Kobe Bryant lauzwa kwa zaidi ya Sh 910 milioni

Koti la Kobe Bryant lauzwa kwa zaidi ya Sh 910 milioni

Koti la marehemu mkali wa mpira wa kikapu, Marekani Kobe Bryant alilolivaa kabla ya mchezo wake wa mwisho wa NBA limeuzwa kwa dola 336,000 ikiwa ni zaidi ya Sh 910 milioni.

Vazi hilo lenye ukubwa wa XL limeripotiwa kununuliwa na mtoto wa tajiri Marekani ambaye hajawekwa wazi jina lake.

Utakumbuka kuwa Black Mamba alilivaa vazi hilo kabla ya kufunga pointi 60 akiwa na timu yake ya Lakes dhidi ya Utah Jazz mchezo uliochezwa katika uwanja wa Staples Center, Aprili 2016.

Koti hilo ambalo liliwekwa pamoja na picha ya nyota huyo ili kuthibitisha, liliwekwa kwenye mnada wa SCP Auctions tangu mwezi Julai.

Kobe Bryant alikuwa mchezaji maarufu wa mpira wa kikapu kutoka Marekani ambaye aliichezea timu ya Los Angeles Lakers katika NBA (Chama cha Taifa cha Mpira wa Kikapu). Alizaliwa mwaka 1978 na alifariki dunia kwa ajali ya helikopta Januari 26, 2020.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags