Kukosea Ni Kujifunza Amini!

Kukosea Ni Kujifunza Amini!

Michael Anderson

Huwa hatupendi kukosea kwa sababu tunachukulia kukosea ni kutokujua na kushindwa.

Lakini kukosea ndiyo mwanzo mzuri wa kujifunza. Unapokosea unakuwa na fursa ya kujifunza kipi kinafanya kazi na kipi hakifanyi kisha kuchukua hatua zilizo sahihi.

Usiache kufanya maamuzi au kuchukua hatua kwa sababu unaogopa kukosea, kukosea ndiyo mwanzo wa kujifunza, jifunze na uweze kuwa bora zaidi.

 

Faida za kukosea kwenye maisha ya kawaida

Faida za kukosea kwenye maisha ni muhimu kuzifahamu na unaweza kujifunza kutokana na makosa mbalimbali unayoyafanya kila mara maishani mwako.

  1. Makosa Hutuonyesha Mambo Tusiyoyafahamu

Ni wazi kuwa makosa mengine hutokea kwa kufanya vitu au maamuzi tusiyoyafahamu vyema. Kwa njia ya makosa hayo tutaweza kufahamu vitu hivyo.

  1. Makosa Hutufundisha Maana ya Mafanikio

Pasipo shaka, mafanikio siyo mteremko au ukamilifu. Mafanikio ni kujifunza kutokana na makosa na kuepuka kuyarudia tena mbeleni.

Kupitia makosa tunaweza kujifunza tufanye nini ili tufanikiwe katika lile tunalolifanya.

  1. Makosa Hutufundisha Kuomba Msaada

Tunapofanya makosa, mara nyingi tunatambua kuwa tunahitaji watu wakutusaidia kuyarekebisha au kutupa ushauri. Kabla ya kufanya kosa ambalo limekuletea matatizo, unaweza kufikiri unajitosheleza au hauhitaji msaada wowote.

  1. Makosa Hutuwezesha Kufahamu Mambo ya Msingi

Inawezekana kosa limetokea kutokana na kufanya au kuzingatia jambo ambalo siyo la msingi. Hivyo kwa njia ya kosa hilo utaweza kubaini mambo ya msingi na yasiyo ya msingi.

  1. Makosa Hutufundisha Umuhimu wa Wengine

Inawezekana umekosea kwa sababu umepuuza nafasi ya watu wengine katika maamuzi au kile unachokifanya. Kwa sababu hii basi utakuwa umefahamu umuhimu wa wengine.

  1. Makosa Hutuonesha Kinachofaa na Kisichofaa

Unapotumia kitu au njia fulani na ikakusababishia kukosea, ni wazi kuwa utakuwa umebaini kuwa kitu au njia hiyo haifai.

  1. Makosa Hutufundisha Thamani ya Msamaha

Ikiwa umemkosea mtu ambaye ni wa thamani kwako, ni wazi kuwa utahitaji kumwomba msamaha ili kuendeleza uhusiano wako na yeye. Hivyo kwa njia ya makosa tunatambua umuhimu wa msamaha.

  1. Hutufundisha Kufanya Uchaguzi Sahihi

Mara nyingi tunakosea kutokana na kufanya uchaguzi mbaya. Hivyo kosa litakufundisha kuwa uchaguzi uliofanya siyo sahihi.

  1. Makosa Hutufundisha Kufanya Majaribio

Unapofanya kosa na kupata matokeo fulani ni sawa na mtu anayefanya majaribio. Hivyo utafahamu matokeo ya kile ulichokifanya kama ni mazuri au mabaya.

  1. Makosa Hutuwezesha Kufanya Chaguzi Nyingine

Inawezekana kuna uchaguzi fulani uliupuuzia au hukufahamu umuhimu na ubora wake. Baada ya kukosea katika uchaguazi ulio uchagua utabaini kuwa uchaguzi ulioupuuzia una nafasi kubwa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags