Nicotrack Ataja Sababu Muziki Wa Zamani Kudumu

Nicotrack Ataja Sababu Muziki Wa Zamani Kudumu

DJ na mwanahabari mkongwe nchini, DJ Nicotrack ameelezea sababu inayosababisha nyimbo za zamani kudumu katika ubora na masikioni mwa mashabiki kuliko za sasa.

Nicotrack amesema uandaaji katika muziki wa zamani na sasa ni tofauti kwani zamani watayarishaji walikuwa na mchango mkubwa kwenye uzalishaji ukilinganisha na sasa.

"Zamani msanii anaenda studio anamsikilizisha idea produza. Produza baada ya kusikiliza anashauri cha kuongeza au kupunguza kisha anamuandalia beat kwa ajili ya kwenda kufanya maandalizi na kumpatia siku za kutosha kwa ajili mazoezi ya kurekodi.

"Msanii akirudi studio kurekodi bado produza ana nafasi ya kufanya uamuzi juu ya utayari wa msanii kama arudie au akajifue zaidi. Baada ya msanii kurekodi produza anajipa muda wa kuuandaa wimbo kwa kushirikiana na watayarishaji wenzake,"anasema na kuongezea.

"Kama atahitajika msanii wa kupiga kiitikio atatafutwa na kama itahitajika gitaa, kinanda ama tarumbeta atatafutwa mtaalam aje apige. Baada ya hapo wimbo utafanyiwa mixing na mastering na mtaalamu wa shughuli hizo kisha ndiyo utatoka tena na hiyo ni baada ya wataalamu wa muziki kuusikiliza na kujiridhisha," amesema Nicotrack.

Anasema muziki wa sasa wasanii wanarekodi kwa mizuka na hata collabo nyingi zinazosikika wasanii na watayarishaji hawafanyi maandalizi ya kutosha kuupika wimbo.

"Muziki wa sasa wasanii wanarekodi kwa vibe tu na hata kolabo nyingi zinazosikika wasanii walikutana studio. Produza mmoja anamaliza wimbo usiku mmoja. wimbo unatrend wiki mbili na kupotea ndani ya mwezi mmoja," amesema Nicotrack.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags