Kwenye Saluni Za Miaka Ya 1940 Mambo Yalikuwa Hivi

Kwenye Saluni Za Miaka Ya 1940 Mambo Yalikuwa Hivi

Miaka ya 1940, kulikuwa na saluni zilizopewa jina la ‘Slenderizing Salons’. Saluni hizo zilipata umaarufu kutokana na wanawake wengi kupendelea kwenda kwa lengo la kupata umbo jembamba huku wakitumia mitambo, kama vile mashine za Rollers na Massagers.

Saluni hizo, ambazo zilikuwa ndio za kwanza kwa ajili ya mazoezi kwa wanawake. Zilikuwa zikisaidia kupunguza uzito, bila ya mazoezi magumu au mlo maalumu huku vifaa hivyo vikijikita katika kuwapa wanawake mwili mwembamba ‘slim’.

Mashine hizo mara nyingi zilihusisha mazoezi yasiyo na juhudi nyingi (passive exercise), ambapo wateja walilala au kukaa huku vifaa hivyo vikitetemesha au kukanda miili yao. Ambapo ilikuwa ikipunguza mafuta mwilini na kufanya ngozi kuwa laini na nyororo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags