Rapa Lil Wayne ametangaza kutohudhuria Half Time Show ya Super Bowl inayotarajiwa kufanyika Februari 9, 2025 kwenye mji aliozaliwa rapa huyo 'New Orleans'.
Wayne amesema kuwa hatohudhuria show hiyo na badala yake kuna kitu maalum ambacho amewaandalia mashabiki wake.
"Siwezi kuwepo pale wiki hii, nawakubali New orleans lakini nipo nafanyia kazi kitu maalum ambacho kitawashangaza," amesema Lil Wayne.
Super Bowl ambayo itafanyika mwezi huu itaongozwa na rapa Kendrick Lamar ambaye ni mshindi wa tuzo tano za Grammy 2025. Kulikuwa na minong'ono huenda Lil Wayne angetokea kama surprise.
Super Bowl huwa ni mchezo wa fainali kati ya timu za Cricket nchini Marekani na hutoa burudani ya muziki muda wa mapumziko, wasanii wengi wakubwa wamefanikiwa kupita kwenye jukwaa hilo ambapo 2024 alitumbuiza Usher Raymond, 2023 alikuwa Rihanna.

Leave a Reply