Lukaku bado hajaonekana kwa Mourinho

Lukaku bado hajaonekana kwa Mourinho

‘Kocha’ wa ‘klabu’ ya Roma, Jose Mourinho amesisitiza kuwa bao la mchezaji Romelu Lukaku lilikuwa siyo muhimu baada ya ‘straika’ huyo kufunga katika dakika ya 82 kwenye ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya ‘klabu’ ya Empoli.

Aidha Lukaku alifunga bao lake la kwanza akiwa na uzi wa ‘timu’ hiyo baada ya kujiunga kwa mkopo akitokea ‘klabu’ ya #Chelsea lakini inadaiwa kuwa ‘kocha’ alionyesha kutokuwa furaha na bao alilofunga mchezaji huyo.

Pamoja na kulipuuiza bao hilo, Mourinho alimsifu Lukaku kuwa alibadilisha upepo kufuatia ushindi huo mkubwa baada ya kuanza msimu kwa kusuasua. Akisema kuwa bao lake halikuwa na umuhimu na anajua ‘mastaika’ wanacheza kwa sababu ya kufunga tu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags