Lulu Diva kumpa fundisho Lavalava

Lulu Diva kumpa fundisho Lavalava

Baada ya mwanamuziki Lavalava kudai kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na mwanadada Lulu Diva na kuwa kwa sasa amebaki kuwa kama dada kwake, msanii Diva amemjia juu Lavalava kwa kumtaka atengue kauli hizo za uongo.

Lulu Diva kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share ujumbe akidai kuwa taarifa hizo zinamchafua hivyo anamtaka Lavalava kusafisha jina lake mara moja iwezekanavyo.


“Imebainika kuwa baadhi ya watu na Media zinahusika kusambaza taarifa za uongo zisizo na msingi kuhusu mahusiano yangu binafsi. Taarifa hizo sio tu kwamba zinachafua jina langu lakini pia zinaharibu heshima yangu katika jamii na kwingineko.

Ninawapa onyo rasmi kuwa mnalo jukumu la kutengua kauli hizo za uongo mara moja. Nawapa muda hadi kesho saa nne asubuhi 22/06/2024 kufanya hivyo. Iwapo hamtatengua kauli zenu ndani ya muda uliotolewa nitachukua hatua za kisheria mara moja ili kulinda haki zangu na heshima yangu” ameandika Lulu Diva

Aidha aliongezea kwa kueleza kuwa amesikitishwa zaidi na kauli za Lavalava dhidi yake alizozitoa kwenye mahojiano yake ya hivi karibuni.

Utakumbuka kuwa wawili hao walihusishwa kutoka kimapenzi wakati wakifanya promo ya ngoma yao ya ‘Samahani’ iliyotoka mwaka 2021.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags