Maisha ya Brian baada ya kuigiza filamu ya Yesu

Maisha ya Brian baada ya kuigiza filamu ya Yesu

Brian Deacon ni jina la mwigizaji maarufu wa Uingereza aliyecheza kama Yesu Kristo katika filamu ya 'Jesus' (1979), iliyoandaliwa na kampuni ya 'Jesus Film Project'.
Filamu hiyo imekuwa mojawapo ya kazi maarufu zaidi duniani yenye kueneza hadithi ya maisha ya Yesu kwa mamilioni ya watu.

Hata hivyo, baada ya kucheza filamu hiyo maisha ya Brian yalibadilika. Alikubali kwamba filamu hiyo ilimletea umaarufu mkubwa, lakini pia ilimleta changamoto. Kwani ilimlazimu kuwa mfano katika jamii na kuishi maisha ya kiroho.

Katika maisha hayo amejikita katika kuhudumia jamii, akifanya kazi na mashirika mbalimbali ya misaada kwa wahitaji na kuzingatia maisha ya kiimani katika dini ya Kikristo akiyaishi mafundisho ya Yesu.

Aidha kwa kuwa alijua alikuwa na nafasi ya kuathiri wengi kutokana na uhusika aliocheza, alitumia umaarufu wake kuhamasisha watu kuwa na imani na kuishi maisha yenye maadili.

Mbali na kuigiza kama Yesu katika filamu hiyo ya 1979, pia ameonekana katika filamu nyingine nyingi, akicheza kama Heumac katika 'The Feathered Serpent' (1976, 1978), Frank Miles(1978) 'Lillie', alicheza na kaka yake, Eric, katika filamu ya Peter Greenaway 'A Zed & Two Noughts' (1985) kama Oswald Deuce.

Mbali na hizo filamu nyingine ni Star Wars: Knights of the Old Republic II – The Sith Lords (2004), The Projectionist (2012), The Night of the Rabbit (2013), Mistaken(2013)



Katika moja ya mahojiano yale aliwahi kusema wakala wake alimshauri asichukue uhusika huo wiki tatu kabla ya upigaji picha za filamu hiyo kuanza. Huku akikazia kuwa alisoma injili ya Luka zaidi ya mara 20.

"Kusoma Biblia kulinisaidia kuona tabia ya Yesu kama mtu mwenye huruma kubwa na uelewa. Tabia ya Yesu ni ya kila mtu, nilipaswa kupata sauti yangu na hisia kwa ajili ya uhusika huo,"alisema

Utakumbuka Deacon alicheza filamu hiyo akiwa na umri wa miaka 30. Na alikuwa miongoni mwa waigizaji 900 waliopimwa kwa ajili ya uhusika huo na mtayarishaji John Heyman. Deacon alizaliwa Februari 13, 1949 huko Uingereza. Hadi sasa filamu hiyo ya Yesu inapatikana kwa lugha zaidi ya 500 ikiwa na matoleo 237.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags