Katika jamii nyingi mtu anayevaa suti huonekana kama mwenye nidhamu na anayejitambua. Kawaida Suti haivutii kwa sababu ya bei yake bali kwa namna inavyovaliwa, inavyotosha mwilini na inavyoendana na tukio husika. Kwa hiyo, kuna mambo kadhaa ya kuzingatia unapotaka kuvaa suti.
Kwanza, suti inapaswa kukutosha vizuri. Suti nzuri huonekana kama imetengenezwa mahsusi kwa mwili wako. Mabega ya koti suti hayapaswi kukubana sana, mikono isiwe mirefu mno na suruali ikae vizuri juu ya kiatu. Suti isiyokaa vizuri huweza kuharibu kabisa mwonekano wako, hata kama ni ya gharama kubwa.
Pili, chagua rangi sahihi kulingana na tukio. Kwa mazingira ya kazi au mahojiano, rangi kama bluu ya bahari, kijivu au nyeusi huwa na mwonekano mzuri. Kwa hafla zisizo rasmi, unaweza kujaribu rangi nyingine lakini bado ukazingatia uwiano wa mavazi.
Tatu, zingatia usafi na mpangilio wa mavazi mengine unayovaa pamoja na suti, kama vile shati, tai, viatu na soksi. Shati safi, tai isiyo na mambo mengi, viatu vya ngozi vilivyosafishwa, na soksi ni vitu vidogo lakini vyenye athari kubwa kwenye mwonekano wako.
Leave a Reply