Manara afunga ndoa na Zaiylissa

Manara afunga ndoa na Zaiylissa

Baada ya kudai kuwa ndao yake na mpenzi wake Zaiylissa, itakuwa ya siri hatimaye Haji Manara amefunga ndoa na muigizaji huyo siku ya leo Jumatato, Januari 24, 2024.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Manara ame-share picha hiyo aikiambatana na ujumbe usemao “Allhamdullillah sasa ni rasmi tutambulike Mr and Mrs Haji Manara”

Ndoa hiyo si ya kwanza kwa Zaiylissa mwaka 2023 alifunga ndoa na mwanamuziki wa singeli Dulla Makabila, na ndoa yao ilidumu kwa mwezi mmoja tu hata hivyo kwa Haji pia siyo ndoa yake ya kwanza kwani aliwahi kufunga ndoa na wanawake kadhaa kama vile Rubynah, Rushaynah na Naheedah, hii itakuwa ni ndoa ya sita kwa Manara kufuatiwa na malezo ya mama yake mzazi wakati alipokuwa anafunga ndoa na Rushaynah.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags