Manara: usimba na uyanga unaharibu timu ya Taifa

Manara: usimba na uyanga unaharibu timu ya Taifa

Oyeeeeeaaah! Likitokea swala la jambo linajumuisha watanzania basi ni vyema wote tukaungana na jambo hilo, basi bwana lile semaji la mabingwa Haji Marana ametoa povu baada ya CEO wa klabu ya simba Barbara Gonzalez baada ya kuandika katika ukurasa wake wa twiter kuwa asilimia 36% ya timu ya taifa ni wachezaji wa simba.

Kauli hiyo ambayo imemkera sana mzee wa byuti byuti kupiutia ukurasa wake wa Instagram alidondosha ujumbe mzito na kusema kuwa “kuna vitu unapokuwa kiongozi hupaswi kusema,inaleta ukakasi na ni ushamba, usimba na uyanga kwenye timu ya taifa ni sumu kubwa kwenye maendeleo ya hii timu,,tumekuwa tunaleta utimu hadi kwenye national team na imetugharimu kwa muda mrefu mno” ameandika Haji Manara

Manara aliendelea kwa kuandika kuwa “Mengine tuwaachie Washabiki Oya Oya wa Mtaani ambao kwao kila kitu ni kutambiana tu,,lakini unapokuwa kiongozi kuna vtu hupaswi hata kuvifikiria. Last Game Wachezaji wengi waliocheza Taifa Stars,walitoka Yanga na hatukuona kiongozi yoyote wa Club hyo akitamba Kwa hilo,,Coz wanapokuwa pale,wote wanakuwa Wawakilishi wa nchi”

“Team yenyewe haipati mashabiki wengi wa kuisapoti Uwanjani ,kisha kiongozi wa Club unaleta ushabiki kisa Wachezaji wa Team yako wengi wamechaguliwa. Ni ile Basi tu mengine hatutaki kusema,,katika hao Tisa kuna wengine hata Game moja hawajacheza msimu huu,,inashangaza hata imekuwaje waitwe kwenye hiyo team.” Ameandika Haji Manara

Aloooooooh! Njoo hapa udondoshe komenti yako hapa chini je anachokisema Manara kiko sahihi au laah!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags